THE LUTHERAN RADIO CENTRE

 

 ANNOUNCEMENTS:

 

 

 

CORONA COVID 19

Corona ni jamii kubwa ya virusi vinavyosababisha maradhi kwa wanyama na binadamu. Kwa binadamu, jamii kadhaa za virusi vya Corona vinafahamika kusababisha maambukizi kwenye njia ya hewa na mfumo wa upumuaji. Maradhi yaliyowahi kusababisha madhara makubwa kutokana na virusi vya Corona ni pamoja na MERS na SARS yaliyozuka mwanzoni mwa miaka ya 2000. Kirusi cha Corona kilichogundulika hivi karibuni kinasababisha ugonjwa unaofahamika kama COVID-19.

COVID-19 NI NINI?

COVID-19 ni ugonjwa wa kuambukiza unaosababishwa na virusi vya Corona. Virusi hivyo vipya havikuwa vikifahamika hapo kabla na sayansi ya tiba. Na vilianzia nchini China mwezi Disemba mwaka 2019.

DALILI ZA CORONA NI ZIPI?

Dalili kuu za Corona ni pamoja na Homa kali, Uchovu na Kikohozi kikavu na zinatokea taratibu. Dalili kubwa na inayoweza kutia hofu, ni mtu kukosa pumzi. Lakini isikutishe, ni mtu 1 pekee kati ya watu 6 walioambukizwa virusi vya Corona hufikia dalili hiyo ya hatari. Na asilimia 80 ya walio na virusi hivyo hupata nafuu bila kuhitaji msaada wa matibabu.

NINAWEZA KUJIKINGA VIPI NA VIRUSI VYA CORONA?

  1. Nawa vizuri na kila wakati mikono yako kwa maji ya vuguvugu, sabuni au dawa za kuua vijijidudu kwa angalau sekunde 20. Kaa umbali wa angalau hatua mbili (2) kutoka mtu anayepiga chafya au kukohoa.
  2. Epuka kushika macho, pua na mdomo kwa mikono isiyo safi kwa sababu mikono hushika sehemu nyingi na ni rahisi kubeba vimelea vya maradhi.
  3. Hakikisha wewe, na walio karibu yako wanazingatia ustaarabu wa kuzuia pua na mdomo wakati wa kukohoa au kupiga chafya.
  4. Baki nyumbani ikiwa hujisikii vizuri. Iwapo una mafua makali, homa, kikohozi na kushindwa kuhema nenda hospitali kwa sababu huko wataalamu watakupatia msaada muhimu.
  5. Epuka kuwa sehemu yenye msongamano, kama vyombo vya usafiri, maduka na maeneo yenye yenye mgandamizo wa hewa.
  6. Nunua kifunika mdomo na pua na kukikavaa ukiwa kwenye mikusanyiko.
  7. Fuatilia taarifa za afya na matangazo yake kuhusu virusi vya Corona.

VIRUSI VYA CORONA VINA TIBA

Hadi sasa hakuna tiba dhidi ya virusi vya Corona lakini chanjo dhidi ya virusi hivyo inapatika, Kupata chanjo ya Corona ni hatua muhimu unayoweza kuchukua ili kujikinga na athari za virusi vta Corona.

 

 

 Announcement 1

 

 Announcement 2
Important Links:    ELCT   LRC Mirror site Tansania   LRC ELCT LRC Backupserver   LWF   RADIO UPENDO DAR   RADIO FURAHA   TWR   Habari Maalum
                                    All Rights Reserved 2019