THE LUTHERAN RADIO CENTRE

 

 ANNOUNCEMENTS:

 

 

 
PROCLAIMING JESUS CHRIST INTO HIS WORLD

NEWS(HABARI)

WANANCHI WASHAURIWA KUTUMIA TEKNOLOJIA YA HABARI KUPATA AU KUTOA TAARIFA ZA AFYA

Chuo Kikuu Kikuu Kishiriki cha Afya na Sayansi Muhimbili (MUHAS) kwa kushirikiana na wadau wa maendeleo yanayohusiana na Afya wamefanya kongamano kuhusu tekinolojia ya habari inavyoweza kuboersha huduma za Afya.

Hayo yameelezwa na Luteni Kanali Dkt. Pius Horumpende Mkurugenzi msaidizi wa tiba kutoka Wizara ya Afya ambaye amesema kwamba wananchi wanaweza kutumia tekinolojia ya habari kupata na kutoa taarifa zinazohusiana na afya kuongeza tija na kuboresha huduma za afya nchini.

Amesema kwamba Wizara ya Afya imejikita katika kutoa huduma bora na huduma hizo zitatolewa kwa njia ya kimtandao ili waweze kufikia watu wengi kwa wakati mmoja, kutoa taarifa kuhusu magonjwa yasiyokuwa ya kuambukizwa kwa kutumia teknolojia ya habari kunaweza kudhibiti magonjwa hayo lakini pia itapunguza gharama zinazoweza kujitokeza endapo taarifa zinaweza kuchelewa kuzifikia mamlaka husika.

"Wito wangu ni kuwasihi wananchi wote waweze kutumia technolojia ya habari kutoa taarifa zozote zinazohusiana na maradhi ya mlipuko au maradhi mengine ili kusaidia kuepusha vifo au gharama zinazoweza kujitokeza baada ya taarifa kuchelewa kufika kwenye mamlaka husika," amesema Luteni Kanali Dkt. Pius Horumpende

Kanali Pius ameongeza kwamba tekinolojia ya habari itasawasaidia wananchi kujua sehemu husika za kwenda kutoa taarifa na kwenda kupata huduma.

Kuhusu taarifa za uhakika amesema wizara inachosisitiza kwa wananchi ni kuhakikisha wanapata taarifa hizo kutoka kwa vyanzo sahihi, Mamlaka au wataalam wa afya ambao wanatambuliwa na wizara ya Afya ili kutopotosha jamii kutokana na taarifa zitakazokuwa zikitolewa.

 

 

 Announcement 1

 

 Announcement 2
Important Links:    ELCT   LRC Mirror site Tansania   LRC ELCT LRC Backupserver   LWF   RADIO UPENDO DAR   RADIO FURAHA   TWR   Habari Maalum
                                    All Rights Reserved 2019