THE LUTHERAN RADIO CENTRE

 

 ANNOUNCEMENTS:

 

 

 
PROCLAIMING JESUS CHRIST INTO HIS WORLD

NEWS(HABARI)

RAIS WA KENYA ASEMA HAKUNA MTU ALIYE JUU YA SHERIA

Rais William Ruto amesema kwamba hatakubali "kutoijali nchi" baada ya maandamano ya ghasia kukumba mji mkuu, Nairobi na mji wa magharibi wa Kisumu.

Maandamano hayo yaliandaliwa na mwanasiasa wa upinzani Raila Odinga ambaye analaumu sera za serikali kwa kuzidisha kupanda kwa gharama ya maisha.

Pia amedai bila ushahidi kwamba alishinda uchaguzi wa urais wa mwaka jana.

"Nitahakikisha kama rais kwamba nchi hii inaongozwa na sheria, na hakuna chochote zaidi ya sheria na katiba kitakachokuwa sehemu ya kile tunachofanya," Bw Ruto alisema.

Rais amemshutumu Bw Odinga kwa kujaribu kuanzisha mgogoro kwa mara ya pili, akisema alifanya vivyo hivyo baada ya uchaguzi wa 2017 na kumlazimisha Rais wa wakati huo Uhuru Kenyatta kufikia makubaliano ambayo yalimpa mapendeleo ya serikali.

Hata hivyo, Bw Odinga amekanusha madai hayo.

 

 

 Announcement 1

 

 Announcement 2
Important Links:    ELCT   LRC Mirror site Tansania   LRC ELCT LRC Backupserver   LWF   RADIO UPENDO DAR   RADIO FURAHA   TWR   Habari Maalum
                                    All Rights Reserved 2019