THE LUTHERAN RADIO CENTRE

 

 ANNOUNCEMENTS:

 

 

 
PROCLAIMING JESUS CHRIST INTO HIS WORLD

NEWS(HABARI)

MASHIRIKA YA HAKI ZA BINADAMU YATAKA IRAN KUSITISHA ADHABU YA KIFO

Mashirika ya kimataifa ya kutetea haki za binadamu yametoa wito wa shinikizo la kimataifa kwa Iran kuacha kutoa hukumu ya kifo kwa waandamanaji wanaoipinga serikali.

Mahakama ya Iran imesema watu watano waliokamatwa katika harakati ya serikali ya kukabiliana na maandamano ya miezi miwili wamehukumiwa kifo tangu Jumapili.

Wafungwa hao watano, ambao hakuna hata mmoja wao aliyetajwa, ni pamoja na watu watatu ambao walihukumiwa kifungo hicho Jumatano.

Katika ujumbe uliotumwa kwa VOA, Mahmood Amiry-Moghaddam, mkurugenzi wa shirika la Haki za Binadamu la Oslo la Iran, alisema serikali ya Iran inatumia hukumu ya kifo kujaribu kuwatia hofu wananchi kwa mara nyingine tena kuogopa mamlaka yake.

 

 

 Announcement 1

 

 Announcement 2
Important Links:    ELCT   LRC Mirror site Tansania   LRC ELCT LRC Backupserver   LWF   RADIO UPENDO DAR   RADIO FURAHA   TWR   Habari Maalum
                                    All Rights Reserved 2019