THE LUTHERAN RADIO CENTRE

 

 ANNOUNCEMENTS:

 

 

 
PROCLAIMING JESUS CHRIST INTO HIS WORLD

NEWS(HABARI)

SERIKALI YA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA KUFANYA SENSA YA MAJENGO KATIKA SENSA YA MWAKA HUU

Kwa Mara ya kwanza serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inakwenda kutekeleza zoezi la sensa ya majengo Katika sensa ya mwaka huu ili kutatua changamoto ya upatikanaji wa Takwimu sahihi za majengo nchini

Faida za upatikanaji wa Takwimu hizo ni ili kufahamu Hali halisi za majengo ya wananchi nchi, kufahamu upungufu wa nyumba , sehemu zenye nyumba zisizo na ubora , kutambua maeneo ya biashara na uwekezaji ili kuwezesha serikali kupanga mipango.

Afisa maendeleo mwandamizi Tumaini Setumbi kutoka wizara ya ardhi amebainisha hayo leo Katika siku ya pili ya mafunzo kwa wahariri wa Redio za mikoani iliyofanyika Katika chuo kikuu kishiriki Cha Elimu Mkwawa Iringa wakati akiwasilisha mada kuhusu sensa ya majengo

Hata hivyo ili kuhakikisha zoezi Hilo linafanikiwa makarani wa sensa wataongozwa na ramani itakayowasaidia kutambua maeneo ya kuhesabu watu ili kuepuka mwananchi yeyote kuachwa Katika zoezi hili au mtu kuhesabiwa zaidi ya Mara moja.

 

 

 Announcement 1

 

 Announcement 2
Important Links:    ELCT   LRC Mirror site Tansania   LRC ELCT LRC Backupserver   LWF   RADIO UPENDO DAR   RADIO FURAHA   TWR   Habari Maalum
                                    All Rights Reserved 2019