THE LUTHERAN RADIO CENTRE

 

 ANNOUNCEMENTS:

 

 

 
PROCLAIMING JESUS CHRIST INTO HIS WORLD

NEWS(HABARI)

UMOJA WA MATAIFA KUCHUNGUZA MASHAMBULIZI YALIYOUWA WAFUNGWA WA KIVITA WA UKRAINE

Umoja wa Mataifa umesema utaanzisha uchunguzi wa mashambulizi dhidi ya gereza moja mashariki mwa Ukraine linaloshikiliwa na Urusi.

Jeshi la Urusi lilisema wafungwa 50 wa kivita waliuawa na wengine 73 kujeruhiwa katika mashambulizi ya wiki iliyopita dhidi ya gereza la Olenivka. Kyiv na Moscow zinashutumiana kwa mashambulizi hayo katika eneo la Donestk. Urusi inasema Ukraine ilifanya mashambulizi hayo kuwazuwia wanajeshi wake kujisalimisha kutokana na kuishiwa na matumaini.

Ukraine inaituhumu Urusi kulishambulia gereza hilo ili kuficha mateso na mauaji yake kwa wafungwa wa kivita wa Ukraine. Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Antonio Guterres, amesema mataifa yote mawili yameomba uchunguzi ufanyike. Ameongeza kuwa hadidu rejea za uchunguzi huo, ambazo zitahitajika kukubalika na pande zote mbili, zinatayarishwa.

 

 

 Announcement 1

 

 Announcement 2
Important Links:    ELCT   LRC Mirror site Tansania   LRC ELCT LRC Backupserver   LWF   RADIO UPENDO DAR   RADIO FURAHA   TWR   Habari Maalum
                                    All Rights Reserved 2019