THE LUTHERAN RADIO CENTRE

 

 ANNOUNCEMENTS:

 

 

 
PROCLAIMING JESUS CHRIST INTO HIS WORLD

NEWS(HABARI)

RAIS SAMIA AFANYA ZIARA YA KIHISTORIA AFRIKA KUSINI AHIMIZA USHIRIKIANO WA KIUSALAMA NA BIASHARA

Rais wa Tanzania Samia Suluhu Hassan katika ziara yake ya kiserikali nchini Afrika Kusini amehimiza ushirikiano zaidi wa kiusalama na biashara kati ya nchi hizo mbili.

Rais Samia amekutana na Rais wa Afrika Kusini Cyril Ramaphosa katika mji mkuu wa Pretoria siku ya Alhamisi ambapo ujumbe wake wa Baraza la Mawaziri ulijadili fursa za biashara na makubaliano yanayowezekana na wenzao wa Afrika Kusini.

Hii ni ziara ya kwanza rasmi ya Rais Samia nchini Afrika Kusini tangu awe rais wa Tanzania kufuatia kifo cha mtangulizi wake John Magufuli mwaka 2021.

"Tumekubaliana kuimarisha ushirikiano wetu katika maeneo ya biashara na uwekezaji ikizingatiwa kuwa Afrika Kusini ni miongoni mwa vyanzo vikuu vya uwekezaji wa moja kwa moja wa kigeni nchini Tanzania," alisema Rais Samia. Aliongeza kuwa utalii na viwanda ni sekta zinazoongoza kwa uwekezaji.

Ramaphosa alisema kiwango cha biashara kati ya Tanzania na Afrika Kusini kinaendelea kuongezeka lakini kinaweza kuboreshwa zaidi.

 

 

 Announcement 1

 

 Announcement 2
Important Links:    ELCT   LRC Mirror site Tansania   LRC ELCT LRC Backupserver   LWF   RADIO UPENDO DAR   RADIO FURAHA   TWR   Habari Maalum
                                    All Rights Reserved 2019