THE LUTHERAN RADIO CENTRE

 

 ANNOUNCEMENTS:

 

 

 
PROCLAIMING JESUS CHRIST INTO HIS WORLD

NEWS(HABARI)

TANZANIA, ZAMBIA ZAKUBALIANA KUREJESHA UHUSIANO

Tanzania na Zambia zimekubaliana kurejesha uhusiano wao ambao miaka ya karibuni ulilegalega, huku viongozi wa mataifa hayo wakikubaliana kuimarisha uhusiano wa kisiasa na kuwaunganisha watu.

Rais wa Zambia Haikendi Hichilema amefanya ziara nchini ikiwa ni mara yake ya kwanza tangu kuingia madarakani ambapo alifanya mazungumzo na mwenyeji wake Rais Samia Suluhu Hassan.

Katika mazungumzo hayo wawili hao wamekubaliana mambo kadhaa ikiwamo kurudisha umoja na mshikamano wa mataifa hayo ambayo yalikuwa na ukaribu mkubwa wakati wa uongozi wa awamu ya kwanza ya Serikali za nchi zote mbili.

Akizungumza hilo Rais Samia amesema Serikali yake na ile inayoongozwa na Hichilema wamekubaliana kurejesha uhusiano wa kihistoria ambao nchi hizo uliziunganisha.

"Tanzania na Zambia ni ndugu hapa katikati uhusiano wetu ni kama ulilegalega sasa tumekubaliana kurudisha udugu wetu ambao umeonekana kupotea. Tunarudisha kwa kuangalia uhusiano wa kisiasa, sisi kama viongozi wa nchi tuwaongoze watu wetu waelewane, washirikiane na kuwa ndugu kama ambavyo waasisi wetu waliona inafaa,".

Suala hilo lilizungumziwa pia na Rais Hichilema aliyeeleza kuwa, "Tunatakiwa kuimarisha uhusiano ulioanzishwa na waasisi wetu, ujirani tulio nao hatuna sababu ya kutengana. Mipaka ya kijiografia isiwe chanzo cha kutenganana uhusiano wetu ni wa asili ukienda Tunduma na Nakonda kuna mwingiliano mkubwa kati ya watanzania na wazambia. Kama tusipowatengeneza mazingira ya ushirikiano basi watadhuriana,".

 

 

 Announcement 1

 

 Announcement 2
Important Links:    ELCT   LRC Mirror site Tansania   LRC ELCT LRC Backupserver   LWF   RADIO UPENDO DAR   RADIO FURAHA   TWR   Habari Maalum
                                    All Rights Reserved 2019