THE LUTHERAN RADIO CENTRE

 

 ANNOUNCEMENTS:

 

 

 
PROCLAIMING JESUS CHRIST INTO HIS WORLD

NEWS(HABARI)

UKAME WAKITHIRI KENYA

Mamlaka ya Kudhibiti Ukame ya Kitaifa ya Kenya (NDMA) imesema katika chapisho lake jipya lkwamba idadi ya Wakenya wanaokabiliwa na uhaba mkubwa wa chakula imefikia milioni 4.35, na msimu mfupi wa mvua wa Oktoba hadi Desemba unakatisha matumaini ya mavuno mengi katika maeneo mengi ya nchi.

Kwa mujibu wa NDMA, watoto 942,000 wenye umri wa miezi sita hadi 59 pamoja na akina mama 134,000 wanaonyonyesha katika kaunti zaidi ya 20 zilizoathiriwa na ukame au nusu kame wana utapiamlo na wanahitaji msaada wa haraka wa kibinadamu.

Kenya inakabiliwa na uhaba mkubwa zaidi wa chakula katika miongo minne iliyopita kufuatia misimu minne mfululizo ya uhaba wa mvua, athari mbaya za janga la COVID-19, pamoja na gharama kubwa ya mafuta na pembejeo za shambani kama mbolea.

 

 

 Announcement 1

 

 Announcement 2
Important Links:    ELCT   LRC Mirror site Tansania   LRC ELCT LRC Backupserver   LWF   RADIO UPENDO DAR   RADIO FURAHA   TWR   Habari Maalum
                                    All Rights Reserved 2019