THE LUTHERAN RADIO CENTRE

 

 ANNOUNCEMENTS:

 

 

 
PROCLAIMING JESUS CHRIST INTO HIS WORLD

NEWS(HABARI)

ASKOFU DKT. FEDRICK SHOO ATOA RAI JUU YA KIWANDA CHA VUGA PRESS

Mkuu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania Askofu Dkt. Fedrick Shoo ametoa rai kwa Askofu wa KKKT-Dayosisi ya Kaskazini Mashariki Mch Dkt. Msafiri Joseph Mbilu kuendeleza jitihada za kukifanya Kiwanda cha uchapishaji cha Vuga Press Publishing House ambacho kihistoria ni cha kwanza kwa uchapishaji Afrika Mashariki kiendelee na uzalishaji.

Mkuu wa Kanisa ameyasema hayo tarehe 02/08/2022 akihitimisha ziara yake katika kiwanda hicho kinacho milikiwa na KKKT-Dayosisi ya Kaskazini Mashariki na kuongeza kuwa kuzingatia historia ya kiwanda hicho na mchango wake katika machapisho jitihada za kupata mashine na mitambo ya kisasa ziendelee kuwepo kwani uwitaji bado ni mkubwa.Kwa upande wa meneja wa kiwanda hicho Mch. Moses Shemweta amemuelezea mkuu wa KKKT kuwa kiwanda hicho cha uchapaji wa maandiko kilianzishwa mwaka 1912 na wamisionari kutoka Ujerumani katika eneo la Vuga Mission mahali ambapo sasa ni Chuo cha Biblia na Kituo cha Mikutano Vuga. Ameongeza kuwa mwaka 1949 kutokana na changamoto ya miundo mbinu ya barabara na umeme kiwanda hicho kilihamishiwa katika eneo la Soni.

Kiwanda cha Vuga Press kilianzishwa hasa kwa kusudi la kuchapa maandiko mbalimbali ya makanisa, japo baadae kilihusika katika kuchapa maandiko ya Serikali hasa miaka 15 ya kwanza baada ya Nchi ya Tanzania kupata uhuru hadi pale Serikali ilipoanzisha kiwanda chake na kuchukua baadhi ya watumishi kutoka kiwandani hapo.

Pamoja na Uchapaji, kiwanda hicho kilikuwa kiwanda pekee kilichotoa mafunzo ya uchapaji (Printing School) ya uhakika kwa vijana wengi hapa Nchini, hadi pale Serikali ilipoanzisha mafunzo hayo katika chuo cha VETA Dar es salaam pia ikitumia wataalamu kutoka Vuga Press. huku katika kiwanda cha Vuga Press mafunzo hayo yalikoma mwaka 2010.

Aidha kiwanda hicho ndipo ilipokuwa ofisi ya maandiko ya KKKT, kabla haijahamishiwa Arusha. Kwa wakati huu wateja wakubwa wa kiwanda hicho ni Dayosisi yenyewe, makanisa mengine, mashirika na taasisi za serikali na watu binafsi ndani na nje ya mkoa wa Tanga.

Vuga Press inaundwa na idara kuu mbili ambazo ni Utawala na Uzalishaji. Utawala: Idara hiyo inahusika na uongozi wa kituo, uhasibu, ukadiriaji wa gharama na masoko. Uzalishaji: Idara hii ina sehemu kuu tatu ambazo ni: Uandaaji -Composition and Designing. Uchapaji.Ujaladiaji na umaliziaji.

Awali kabla ya msafara wa Mkuu wa KKKT kufika katika kiwanda hicho Mkuu wa KKKT Dkt. Fredrick Onael Shoo aliagana na uongozi wa KKKT - Dayosisi ya Kaskazini Mashariki, wafanyakazi wa Ofisi Kuu katika Ofisi za Makao Mkuu ya Dayosisi.

 

 

 Announcement 1

 

 Announcement 2
Important Links:    ELCT   LRC Mirror site Tansania   LRC ELCT LRC Backupserver   LWF   RADIO UPENDO DAR   RADIO FURAHA   TWR   Habari Maalum
                                    All Rights Reserved 2019