Kipindi hiki husikika kila siku ya Jumamosi na Jumapili saa tatu kamili hadi saa nne kamili usiku. (21:00-22:00).
Kipindi hiki ni cha mafundisho ya Neno la Mungu ambayo hutolewa na Mwalimu wa Neno la Mungu Nchini Tanzania Christopher na Diana Mwakasege.
LENGO LA KIPINDI HIKI:
Kuwafundisha watu Neno la Mungu kwa usahihi kama Mungu alivyomwita katika huduma yake ya ualimu kati ya huduma tano Mungu alizoziweka katika kanisa.
SOMA
Waefeso 4:11-1211 Naye alitoa wengine kuwa mitume, na wengine kuwa manabii; na wengine kuwa wainjilisti na wengine kuwa wachungaji na waalimu;
12 kwa kusudi la kuwakamilisha watakatifu, hata kazi ya huduma itendeke, hata mwili wa Kristo ujengwe;
Msimamizi wa kipindi hiki ni Ndugu Ezra John.
Kwa maswali kuhususiana na kipindi hiki wasiliana naye kwa simu Namba: 0754518757 au 0658528757.



