THE LUTHERAN RADIO CENTRE

 

 ANNOUNCEMENTS:

 

 

 

USALAMA BARABARANI

Kipindi hiki husikika siku ya Jumatano kuanzia saa nane kamili mchana hadi saa tisa alasiri (02:00-03:00) na kurudiwa usiku saa tano na robo kila jumatano.

Lengo la kipindi hiki:

  1. Kuelimisha wasikilizaji juu Sheria ya Usalama barabarani na kanuni na taratibu ambazo zimewekwa kwa ajili ya watumiaji wa barabara ili kufanya matumizi ya barabara kuwa ya tija na manufaa.
  2. Wasikilizaji kufahamu Sheria zilizowekwa kuepusha makosa ambayo yatasababisha hasara ya miundombinu na hasara juu ya maisha ya watu na mali zao wanapotumia barabara.

Baadhi ya makosa yaliyoanishwa kwenye Sheria ya Usalama Barabarani;

  1. Kuendesha gari au chombo cha moto ambacho hakijasaliwa na Mamlaka husika;
  2. Kushindwa kutembea kwenye chombo cha moto na hati ya usajili wa chombo hicho
  3. Kutumia chombo cha moto kwa ajili ya kufundishia pasipo kufanyiwa usajili na kutambuliwa kama ni chombo kwa ajili ya mafunzo (kuweka alama ya "Learner")
  4. Kushindwa kusimama kwenye kivuko cha reli
  5. Kuendesha gari taratibu sana pasipo sababu yoyote ya msingi. n.k

Haya ni baadhi ya makosa yanayoainishwa na Sheria ya Usalama Barabarani, yapo makosa mengi ambayo tunakutana nayo kila siku.
ili kufahamu yote haya usikokose kusikiliza kipindi cha USALAMA BARABANI kupitia Redio Sauti ya Injili jumatano saa nane kamili mchana.

 

 

 Announcement 1

 

 Announcement 2
Important Links:    ELCT   LRC Mirror site Tansania   LRC ELCT LRC Backupserver   LWF   RADIO UPENDO DAR   RADIO FURAHA   TWR   Habari Maalum
                                    All Rights Reserved 2019