| THE LUTHERAN RADIO CENTRE TANZANIA
PROCLAIMING JESUS CHRIST INTO HIS WORLD

IBADA YA MAZISHI YA BABA CALVIN K. LYARO TAREHE 11/01/2018

"Nimevipiga vita vilivyo vizuri,mwendo nimeumaliza,Imani nimeilinda;

HISTORIA YA MAREHEMU BABA YETU CALVIN KIMANGANO LYARO

KUZALIWA

Baba yetu Calvin Kimangano Lyaro alizaliwa tar.9/10/1942 katika kijiji cha Sembeti Marangu,akiwa mtoto wa pili(2)kati ya watoto sita wa Marehemu Mzee Thomas Kimangano lyaro na mama Eliainaso Morio-lyaro.

KUBATIZWA:

Baba yetu mpendwa alibatizwa tarehe 1 january 1958 katika Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzani Usharika wa Ashira hivi sasa ni Usharika wa Sembeti Marangu.

ELIMU:

Mnamo mwaka 1954 baba yetu mpendwa calvin lyaro alipata elimu ya msingi katika shule ya Mengeni(Native Athourity) na kuhitimu darasa la nne.Baadae aliendelea na "Middle school"katika shule ya Nanjara hadi alipohitimu darasa la nne mwaka 1960.Baadae alijiunga na Sekondari ya Old Moshi kuanzia mwaka 1961 hadi 1964 na kuhitimu kidato cha Nne.Kisha alichaguliwa kujiunga shule ya Sekondari ya juu ya Azania mwaka 1966 hadi 1967 na kuhitimu kidato cha sita. Mnamo mwaka 1967 aliajiriwa na Redio Voice of the GOspel(sauti ya Injili)kama Afisa Mipango Msaidizi wa utangazaji(Assistant Radio Producer). Mkurugenzi wa kituo alikuwa Mchungaji.Efrahim Amos Lyimo. Marehemu baba yetu na mama yetu walipokea wito wa umisionari kwenda Addis Abba Ehtiopia kuendelea na kazi za utangazaji katika kituo cha Radio Voice of the Gospel ambapo walihudumu hadi mwezi Agust 1973 ambapo walirudi Tanzania kuendelea na kazi hiyo hiyo kama afisa Mipango Mwandamizi. Mwaka 1978, baba yetu alijiunga na Chuo Kikuu cha Daystar,Nairobi Kenya ambapo alipata stashahada ya Uandishi wa Habari na utangazaji ambapo alihitimu mwaka 1979.Kisha aliendelea na masomo ya shahada ya kwanza (BA Christian Communication) na ya Pili (MA in Christian Communication)katika hicho chuo cha Daystar hadi alipohitumu mwaka 1992.

UTUMISHI:

Baba yetu mpendwa Calvin lyaro aliporejea masomoni aliendelea na utumishi wake kwenye Kanisa la Kiinjili la kilutheri Tanzania kituo cha Radio Sauti ya Injili.Mnamo mwaka 1995 aliteuliwa kuwa kaimu Mkurugenzi wa kituo na baadae althibitishwa kuwa Mkurugenzi wa kwanza Radio Sauti ya injili asiye Mchungaji kwa mwaka 1997 hadi alipostaafu kwa hesima Desemba 2010. Pia alitumikia Kanisa,Usharika wa Rau kama Mjumbe wa Baraza la Usharika,Mwenyekiti Kamati ya jengona Mwenyekiti kamati ya Fedha kuanzia 2010 hadi alipoagwa rasmi 01/01/2017.

NDOA:

Baba yetu Mzee Calvin Lyaro alifunga Ndoa Takatifu na Felistas Elia MremiTarehe.25/04/1970 huko Marangu Sembeti. katika uhai wake,baba na Mama walijaliwa Kupata watoto watano(5) Wakiume wawili(2)na wakike watatu(3).

UGONJWA NA MAUTI:

Mnamo Nov 2014 Mzee Calvin Lyaro alianza kusumbuliwa na maradhi ya shinikizo la juu la damu,sukari na kiharusi.Ugonjwa uliendelea kuongezeka na kuwa saratani.Alipata matibabu katika hospitali za Kairuki Dar Es salaam,Seliani na Momela Arusha,Mawenzi KCMC zahanati ya SIIMA Moshi na kituo cha Afya cha Katoliki Mbokomu hadi alipofariki tarehe 06 januari 2018 8:45 alasiri. Baba yetu mpendwa Calvin Lyaro ameacha mjane,watoto wanne(4)na wajukuu sita (6)

SHUKRANI:

Tunapenda kuwashukuru Madaktari na wauguzi wote katika haspitali na vituo vyote vya afya aliyopata matibabu.Vile vile tunatoa shukrani kwa Wachungaji Wainjilisti,parishi worker,wanakwaya,wazee wa kanisa na washarika wote wa Usharika wa Rau kwa moyo wao wa upendo na kujitoa kwa dhati kwa familia ya mzee Calvin Lyaro hasa katika kipindi chote cha ugonjwa mpaka alipofariki mzee. pia tunashukuru watumishi wote,Maaskofu,wachungaji,wainjilisti,Parishweka,masista,mapandri na watumishi wengine wote wa Kanisa la Kiinjili la kilutheri Tanzania na makanisa mbalimbali na Parokia zote waliojitoa kwa namna moja au nyingine katika kumfariji na kumwombea mzee katika kipindi chote cha ugonjwa, Mwisho tunatoa shukrani kwa watu wote ndugu jamaa,marafiki na majirani kwa upendo waliouonyesha kwa kujitoa kwa hali na mali katika kipindi chote cha ugonjwa wa mzee Calvin Lyaro.

MUNGU AWABARIKI SANA.

UMEPIGA VITA VILIVYO VYEMA,MWENDO UMEUMALIZA IMANI UMEILINDA.

PUMZIKA KWA AMANI BABA YETU MPENDWA CALVIN LYARO.