Program Contributors Meeting

28.11.2005

Hii ni Sauti ya Injili kupitia Trans World Radio

Askofu.jpg (13130 bytes)

Baba Askofu Gideon G. Maghina akifungua kwa sala kikao cha wachachangia vipindi kilichoandaliwa na REDIO SAUTI YA INJILI

Philemon.jpg (9892 bytes)

Mratibu wa vipindi vya FM,Bwana Philemon Mark Fihavango akiwaelezea wachangia vipindi, utaratibu wa vipindi Redio Sauti ya Injili. (RSYI PROGRAMME CRITERIA)

Lyaro.jpg (9036 bytes)

Mkurugenzi wa Redio Sauti ya injili,Bwana Calvin K Lyaro,akiwasomea Wachangia Vipindi utafiti alioufanya kuhusu wasikilizaji.(THE AFRICAN RADIO AUDIENCE: Some Observations)

Lyatuu.jpg (9128 bytes)

Mama Judith Lyatuu (kushoto) akiwa na baadhi ya Wachangia Vipindi .

TWR.jpg (6764 bytes)

Bwana David Ang`ang`o wa TRANS WORLD RADIO,akiwaeleza washiriki kuhusu kukuza na kuboresha uhusiano (Strengthening Relationships)

Arusha.jpg (9038 bytes)

Mmoja wa washiriki kwenye semina hiyo.

Nairobi.jpg (9404 bytes)

Mmoja wa washiriki akitoa hoja zake .

Kitange.jpg (6279 bytes)

Mwenyekiti wa Bodi ya Redio Sauti ya Injili, Bwana Seth Kitange akifunga semina ya wachangia vipindi Redio Sauti ya Injili.

Tea1.jpg (16657 bytes)

Baadhi ya wafanyakazi wa RSYI walioshiriki kwenye semina ya Wachangia Vipindi Redioni.

Baadhi ya wafanyakazi wa RSYI na wachangia vipindi, wakinywa chai na kubadilishana mawazo.

Tea3.jpg (17009 bytes)

Wachangia Vipindi wa RSYI wakibadilishana mawazo wakati wa chai.

Tea4.jpg (16898 bytes)

Wachangia Vipindi na Wafanyakazi wa RSYI wakinywa chai.

(SWAHILI DESCRIPTION)

Semina ya Wachangia Vipindi iliyoandaliwa na REDIO SAUTI YA INJILI ilifanyika kwenye ukumbi wa Umoja Hostel uliopo Mjini Moshi.Katika sala ya kufungua semina hiyo,Askofu Gideon G. Maghina alisema, habari ni muhimu katika maisha ya watu, na nchi isiyowapa watu wake habari inawanyima haki.

Naye Mkuu wa Dayosisi ya Kaskazini KKKT, Askofu Martin F. Shao,wakati akifungua semina hiyo alisema,RSYI imekuwa ni changamoto kubwa katika kuleta maendeleo kanda ya kaskazini hususani katika elimu, mahospitali na kwenye kilimo.

Pia, Mratibu wa RSYI Bwana Philemon Mark Fihavango aliwaeleza Wachangia Vipindi,kuleta vipindi kwa wakati,kuvihakiki,kuepuka uchochezi na ubaguzi, wakati wanapoandaa vipindi vyao.Pia alisema, mfumo wa kurusha vipindi RSYI kuwa, 70% ni vipindi vya maendeleo,na 30% ni vipindi vya dini.

Hii ni Sauti ya Injili kupitia Trans World Radio

Aidha,Mkurugenzi wa RSYI,Bwana Calvin K.Lyaro alisema,mtayarishaji wa kipindi ni lazima amjue msikilizaji wake anahitaji nini?na pia aulinde na kuutetea utamaduni wa Afrika na kuacha kuiga yale ya nchi za Magharibi.

Akichangia mada kuhusu kukuza na kudumisha uhusiano,Bwana David Ang`ang`o kutoka TRANS WOLRD RADIO (TWR) Kenya alisema, kujenga ushirikiano unahitaji umwelewe mshirika wako na malengo yake,yale mazuri kuyaendeleza na kurekebishana makosa.

Nao Wachangia Vipindi kwa wakati tofauti wakiongea kwenye semina hiyo, waliishukuru RSYI kwa kuwarushia vipindi vyao hewani,na watu wameelimika kutokana na matangazo na vipindi wanavyovirusha kupitia Redio Sauti ya Injili.

Akihitimisha semina hiyo,Mwenyekiti wa Bodi ya RSYI,Bwana Seth Kitange aliipongeza RSYI kwa utamaduni wa kuwaunganisha wanaochangia muda wa hewani,na kutoa rai kuwa waendelee kukutana mara kwa mara na hata ikiwezekana watoe TUZO (zawadi) kwa mtayarishaji bora wa vipindi.

Hii ni Sauti ya Injili kupitia Trans World Radio

Bwana Kitange alitoa hoja nne ambazo zinaweza kuboresha uhusiano na ushirikiano nazo ni:

(1)Wigo upanuliwe ili kuruhusu watayarishaji binafsi, ambao itakuwa ni njia ya kugundua vipaji vipya na kuviboresha.

(2)Kuunda UMOJA kila atakae awe mwanachama,kwa lengo la kutoa mafunzo na kubadilishana mawazo

(3)Kushirikiana na Mashirika mengine hasa ya Redio ili ujumbe ufike kwa watu wote.

(4)Vipindi viwe naUbora na vinavyoelezea vitu bayana ili msikilizaji aelewe kwa ufasaha.

Alisema, "Muwe na ajenda ya kuboresha uhusiano wa kukutana ili kuwe na ushirikiano mzuri wa mawasiliano ili redio iwe nzuri zaidi.

Hii ni Sauti ya Injili kupitia Trans World Radio

elct.jpg (3412 bytes)

Evangelical Lutheran Church in Tanzania

back to start page